Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sheikh Muhammad Yaqubi, mmoja wa maulamaa wa Iraq, alitoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa mwanazuoni mchamungu Ayatollah Sayyid Muhammad Baqir Musawi Kashmiri Najafi.
Ujumbe huu umetolewa kujibu barua ya shukrani kutoka kwa familia na wafiwa wa marehemu Ayatollah Kashmiri, waliotoa pongezi kwa ofisi ya Ayatollah Yaqubi kwa kuandaa kikao cha kumuombea marehemu mwanazuoni huyo mjini Najaf Ashraf.
Katika sehemu ya barua ya wafiwa imesea:
"Kufanyika kwa kikao cha kumuombea marehemu kutoka upande wenu kulituliza majonzi yetu, na hatua hii ya heshima ilikuwa ni dhihirisho la uhusiano wa kina wa kielimu na kiroho miongoni mwa maulamaa."
Kabla ya hapo, Taasisi ya Tabligh ya Kiislamu iliyo chini ya ofisi ya Ayatollah Yaqubi, ilikuwa imeandaa kikao kilichohudhuriwa na mamia ya wanavyuoni na wanafunzi wa elimu za dini kutoka mataifa mbalimbali, kwa ajili ya kuomboleza kuuawa shahidi kwa Ayatollah Sayyid Muhammad Sadr na kufariki kwa Ayatollah Sayyid Muhammad Baqir Musawi Kashmiri.
Matni ya ujumbe wa salamu za rambirambi wa Ayatollah Yaqubi ni kama ifuatavyo:
Bismillāhir-Rahmānir-Rahīm
Watoto na wafiwa wa Hadhrat Allāmah Sayyid Muhammad Baqir Musawi Kashmiri (Rahimahullāh Taʿālā),
Assalāmu ʿalaykum wa raḥmatullāhi wa barakātuh
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia na kutufanikisha kuandaa kikao cha maombolezo kwa ajili ya marehemu wetu mpendwa kando ya kaburi tukufu la Amirul-Mu’minin (ʿalayhis-salām). Hatua hii ilikuwa ni sehemu ya wajibu kutokana na mchango wa kielimu na kivitendo wa marehemu ambaye maisha yake yote aliyatumia kwa ajili ya kuinua dini na kulea wanafunzi wa elimu za dini.
Msiba huu mkubwa wa kumpoteza mwanazuoni huyu mwenye athari njema umetufikia pamoja nanyi wapendwa, na uwepo wenu wenye baraka umetupa faraja. Tunatumaini kuwa nyinyi, kama warithi stahiki wa baba yenu, mtaendeleza njia yake. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa neema akulindeni chini ya hifadhi Yake.
Was-salāmu ʿalaykum wa raḥmatullāhi wa barakātuh
Muhammad al-Yaʿqubi – Najaf Ashraf
Inafaa kutajwa kuwa Ayatollah Sayyid Muhammad Baqir Musawi Safawi alikuwa ni mmoja wa maulamaa wa mkoa wa Kashmir nchini India, na miongoni mwa wanafunzi wa Hawza ya Najaf, pia alikuwa ni mwanafunzi wa Ayatollah Sayyid Abulqasim Khoei na Ayatollah Sayyid Ali Sistani.
Maoni yako